Project Name: Tovuti za Mikoa
Programu hii itakuwezesha kufikia habari za mikoa ya Tanzania bara, ukiwa na programu hii hautahitaji kuandika viunga vya tovuti za mikoa, bali utatakiwa kubofya kwenye jina la mkoa unaotaka kuona habari zake. Hivyo programu hii itawawezesha watumiaji wengi wa simu janja kuwa karibu zaidi na taarifa, fursa, matukio na habari zinazotokea katika mikoa yao na mikoa mingine. Hii itasaidia ufikiaji wa taarifa kuwa rahisi kwa watanzania wengi. Ipakue programu hii na ufurahie fursa, habari na matukio katika mikoa ya Tanzania.